Jan 14, 2011

MCHEZO MCHAFU

HUKU skendo ya watayarishaji wa sinema Bongo kuwarubuni wasichana kufanya nao ngono ikiwa bado haijapoa, orodha ya wasanii waliofanya mchezo mchafu wakati wa kurekodi ‘muvi’ mpya hivi karibuni imewekwa kweupe, makabrasha ya Ijumaa yamebeba ripoti kamili.

Gazeti lenye heshima tele mbele ya ulimwengu wa mastaa, Ijumaa linadhubuthu kuanika kwamba, wasanii wenye majina makubwa Bongo, Vincent Kigosi a.k.a Ray, Mahsein Awadh ‘Dokta Cheni’, Irene Uwoya ‘O’Prah’, Juma Chikoka na chipukizi wa kike katika ‘fildi’ hiyo, Nice Chande wameingia moja kwa moja kwenye listi ya waliofanya uchafu wakati wa kurekodi sinema.
Yamekuwepo madai ya muda mrefu kuhusu uchafu unaofanywa na wasanii wanapokuwa sehemu za kurekodia (location) lakini wenyewe wamekuwa wakikanusha vikali.

Hata hivyo, katika kile kilichoonekana kukikimbilia kivuli chao mwenyewe, hivi karibuni Kampuni ya RJ Company Ltd, iliyo chini ya Mkurugenzi, Vincent Kigosi ‘Ray’, imedhihirisha hilo kwa kutoa sinema iitwayo My Dreams (Ndoto Zangu) ‘Part III’ ikiwa imeonesha kipande chenye uchafu uliofanyika wakati wa kurekodi (behind the scene).

Katika kipengele hicho kuna ushahidi tosha unaoonesha wasanii hao walivyofanya vitendo vichafu huku maneno yenye matusi yakisika moja kwa moja.
Katika sehemu zinazotia kichefuchefu ni pale msanii chipukizi wa kike, Nice Chande, alipoonekana akipanda kitandani na taulo, kisha Juma Chikoka akawa anamrukia na kumshikashika mwilini.
Nice akiwa kitandani, hakuonekana kukasirishwa na kitendo kile, badala yake alikuwa akicheka huku akimzomea Chikoka kabla ya kusikika akimtukana: “Bwana mi’ sitaki, acha u***ge bwana.”

Baadaye Nice alijifunika shuka moja na Dokta Cheni, lakini Cheni alipotoka kwenye shuka hilo alionekana kupatwa na mfadhaiko, na kama hiyo haitoshi, kamera ‘ika-zoom’ (kukuza picha kwa karibu) na kuonesha jinsi msanii huyo alivyokuwa akijishika sehemu nyeti.

Katika ‘love scene’ nyingine, Nice alionekana akiingia kwenye shuka akiwa amevaa nguo ya kulalia, lakini walipofunikwa shuka, akavuliwa nguo hiyo na msanii mmoja wa kiume.

Wakati Nice akiwa kitandani, ndani ya shuka moja na Cheni, akisitiriwa na nguo ya ndani na sidiria, Ray ambaye ndiye Mwongozaji wa filamu hiyo, alisikika akimwambia Nice: “Unaogopa nini, si umevaa ch*p*?”
Vitendo hivyo vinavyoonekana vinathibitisha habari ambazo magazeti pendwa yamekuwa yakiandika mara kwa mara kuhusu uchafu unaofanywa na wasanii wa filamu wakiwa sehemu za kurekodia.

Hivi karibuni, gazeti ndugu na hili, Ijumaa Wikienda toleo namba 162 la Jumatatu Juni 07, 2010 liliandika habari yenye kichwa ‘OH KANUMBA!’ ambayo ilieleza madai ya msanii Steven Kanumba kula denda karibu na wasanii wote wa kike anaoigiza nao kwenye vipande vya kimapenzi.

Aidha, gazeti hilo hilo toleo namba 164 la Jumatatu Juni 28, 2010 liliandika stori yenye kichwa kilichosomeka ‘Jamani Aunt Ezekiel ANATISHA’ ambayo ilielezea jinsi msanii huyo anavyokiri kula denda na baadhi ya ya wasanii wa kiume anaoigiza nao kwenye ‘love scene’, jambo ambalo wataalam wa afya walilielezea kwamba ni hatari kiafya.

Vitendo hivyo moja kwa moja vinaweka wazi viashiria visivyofaa katika ‘fildi’ hiyo ambayo inazidi kupanda chati kila kukicha.

Katika mahojiano na gazeti hili, Onesmo Ngowi, mkazi wa Mwananyamala, Dar, alisema nyuma ya pazia ya sinema ya My Dreams ni chafu na haikupaswa kuoneshwa kwa jamii.

“Jamii inajifunza nini pale, kama siyo uchafu? Hivi unaweza kukaa na mzazi wako sebuleni mkaangalia mambo kama yale?” Alihoji Ngowi.

Mchangiaji mwingine ambaye ni mdau mkubwa wa sinema Bongo, aliyeomba kufichwa jina lake, alisema Ray ametoa tafsiri isiyo sahihi kwa jamii juu ya neno ‘Behind the Scene’.

“Unajua Behind the Scene haijaanzia hapa kwetu, hata kwenye filamu za nje ipo, lakini mara nyingi huonekana matukio ambayo yalirekodiwa wakati wasanii wakifanya mazoezi ya utangulizi kabla ya kuanza kurekodi.
“Siyo matukio kama yale, jamii yetu inajifunza nini kupitia kipande kile, hakuna cha maana ni uchafu mtupu,” alisema na kuongeza:

“Kazi za fasihi ni kuburudisha, kufundisha na kuelimisha, kuonya na kadhalika, lakini pale wametoa burudani gani? Kwahiyo hapakuwa na matukio mengine ya kuwaonesha hadhira zaidi ya yale. Tunakwenda wapi Watanzania. Kwakweli wanapaswa kubadilika.”

Akiongea kwa uchungu, mchangiaji mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Juma Bakari, mkazi wa Msasani, Dar, alisema siku akisikia mke wake anataka kuingia kwenye filamu ndiyo siku atakayompa talaka.
“Atanidanganya nini kama wasanii wenyewe wanatukana, hawana lugha nzuri, wanakaa uchi, wanashikanashikana, ni sanaa ya aina gani hiyo?” Alihoji Juma.

Akizidi kupigilia misumari, msanii mmoja wa filamu nchini ambaye aliomba hifadhi ya jina lake, alisema hakushangaa kuona uchafu ule kwenye ‘Behind the Scene’ ya sinema ile, lakini alimshangaa kuacha kwa kipande kile kionekane.

Hivi karibuni msanii mmoja wa kiume, aliyekuwa akiwika katika Kundi la Shirikisho Msanii Afrika (jina tunaminya) alielezea uozo unaofanyika katika sehemu za kurekodia, alipofanya mahojiano maalum na gazeti moja linalotoka mara mbili kwa wiki (siyo la Global).

Katika habari hiyo, msanii huyo alisema, kumruhusu mke au mchumba wako kucheza sinema ni hatari, vinginevyo moyo huo wa upendo uliomruhusu kushiriki basi utumike kuongozana naye hadi sehemu wanazorekodia.

KUTOKA KWA MHARIRI
Tasnia ya filamu ni pana na inazidi kukua siku hadi siku. Inapendwa na wengi, hivyo ni vyema watayarishaji kuwa makini kabla ya kuingiza sinema sokoni.
Tanzania ni nchi yenye maadili mema na wasanii wanatakiwa kufahamu, wao ni kioo cha jamii, wanaopaswa kulinda na kuheshimu maadili ya Kitanzania.

No comments: